HALMASHAURI YA MJI MAFINGA YAPOKEA PIKIPIKI KWAAJILI YA KUBORESHA SEKTA YA MISITU
Jumla ya pikipiki 12 zenye thamani ya shilingi Milioni 120 zimetolewa na Panda Miti Kibiashara kwaajili ya kuboresha huduma za Ugani ikiwemo kufanya doria kwenye mashamba, kutoa taarifa za moto, kutunza vyanzo vya maji na kudhibiti moto katika Halmashauri 10 zinazofanya kazi na Mradi huu Tanzania.
Akizungumza Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Saad Mtambule amepokea pikipiki 3 kwaajili ya Halmashauri ya Mji Mafinga, Halmashauri ya Mufindi na Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo kwa niaba.Amesema Mazao yatokanayo na Misitu ni moja ya kianzia kikubwa cha Mapato kwa Halmashauri za Mafinga Mji na Halmashauri ya Mufindi.
“ Sekta ya Misitu inatupa sana faida, lakini changamoto kubwa ni namna ya kupanda miti na kudhibiti uchomaji wa moto, jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya nchi na kushusha mapato ya Halmashauri. Hivyo elimu izidi kutolewa kuhusu upandaji wa miti wa kitaalamu na madhara ya moto “.
Akizungumza Mshauri wa Kiufundi wa Mpango Bwana Michael Hawkes amesema kuwa Mpango umesaidia kuongeza uzalishahi bora wa miti kwa wakulima waliopata mafunzo na kugundua viashiria vya moto na namna ya kujikinga na moto. Amesema Mradi wa Panda Miti Kibiashara awamu ya pili umetekelezwa kwenye Halmashauri 10 na wananchi wamepewa elimu mbalimbali ambayo hata mradi ukiisha Mwezi wa 10/ 2023 wananchi wataendelea kuitumia elimu hiyo kwa vizazi vijavyo na Uchumi Endelevu.
Katika hafla hiyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi Happiness Laizer amemuhakikishia Mkuu wa Wilaya na Uongozi wa Panda Miti Kibiashara kuwa Chombo hicho kitatunzwa na kutumika kwenye kazi kusudiwa tu hasa Doria kwenye sekta ya mazao ya misitu.
Akipokea pikipiki hiyo yenye namba za usajili DFP 9187 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Mheshimiwa Regnant Kivinge amesema kuwa kwa Halmashauri ya Mji Mafinga mradi wa PandaMiti Kibiashara umesaidia vijana wengi kupata taaluma ya kupanda miti hasa ukizingatia kuwa moja ya uchumi mkubwa wa wananchi wa Mafinga ni mazao ya misitu.
Akithibitisha umuhimu wa chombo hicho Mratibu wa Panda Miti Kibiashara upande wa Mji Mafinga Bwana Demitrus Kamtoni amesema kuwa uwepo wa pikipiki hiyo utasaidia kuboresha huduma za ugani kwenye mazao ya misitu ikiwemo kufanya doria kutoa Elimu mara kwa mara ya madhara ya moto, kulinda vyanzo vya maji na kudhibiti wizi wa mazao ya misitu.
Mratibu wa PandaMiti Kibiashara Awamu ya tatu Mafinga Bwana Nyachia Roberts amesema kuwa Mradi huu umetekelezwa kwa muda wa miaka minne na utakamilika mwezi wa Oktoba 2023 ambapo umetekekezwa katika Halmashauri 10 , kwa mkoa wa Iringa Mradi unatekelezwa katika Halmashauri ya Mji Mafinga, Mufindi na Kilolo. Aidha mradi umekabidhi vifaa vya kukata matawi ya miti(misumeno 97)kwa kila Halmashauri.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI- MAFINGA TC
Sima Bingileki
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini- MafingaTc
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.