Halmashauri ya Mji Mafinga tarehe 27/10/2023 imesaini mikataba miwili ya lishe ya miaka 8 ngazi ya jamii ambayo ni baina ya Mkurugenzi wa Mji Mafinga na Watendaji wa Kata na mkataba wa pili ni baina ya Watendaji wa Kata na watendaji wa mitaa na Vijiji.
Akizungumza Afisa Lishe Halmashauri ya Mji Mafinga Ndugu Salum Atlas amevitaja viashiria vya Utekelezaji wa Mikataba hiyo kuwa ni:-
-Asilimia ya vikao vya maendeleo ya Kata vilivyofanyika kujadili agenda ya lishe kwa robo ya kwanza.
-Asilimia ya Vijiji/ Mitaa iliyotekeleza maadhimisho ya Siku ya Afya na Lishe ya Mitaa.
-Asilimia ya Mitaa iliyowasilisha taarifa za utekelezaji wa afua za lishe ngqzi ya jamii.
Ameongeza kuwa katika kulifanikisha suala la mikataba ya lishe kwa kipindi cha robo ya kwanza jumla ya wakazi 740 wa Halmashauri ya Mji Mafinga wameweza kupatiwa elimu ya
Lishe kupitia mikutano ya hadhara katika mitaa na kata.
Elimu iliyotolewa ni umuhimu wa Lishe bora, matumizi ya chumvi iliyoongezwa madini joto na uhifadhi wake, makundi matano ya vyakula na mlo kamili.
Akifungu kikao hicho cha Tathmini ya Mkataba wa Lishe Ndugu Robert Kilewo Afisa Tawala Wilaya ya Mufindi akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Mufindi
Mhe. Dkt. Linda Salekwa amesema muhimu elimu ya Lishe izidi kutolewa na matumizi na utunzaji
Sahihi ya chumvi yenye madini joto ili kuhakikisha watoto wetu wanapata
Lishe bora na virutubisho muhimu
Kwa kina mama wajawazito, ili
Kuepukana na utapiamlo .
Kikao hicho kimehudhuriwa na Watendaji wa Kata zote 9 za Halmashauri ya Mji Mafinga Kaimu Mkurugenzi ambaye Ni Katibu wa Kikao Dr. Boviventura Chitopella pamoja na wakuu wa Divisheni.
Imeandaliwa na
Sima Bimgileki
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini- Mafinga TC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.