Jumla ya Tsh, 340,153,629.78/-zimetolewa na Halmashauri ya Mji Mafinga kwaajili ya Mikopo kwa vikundi 33 vya wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu kwa kipindi cha Oktoba-Disemba 2022/2023.
Akikabidhi mfano wa hundi kwa wanavikundi hao Katibu Tawala Wilaya ya Mufindi Ndugu, Servi Ndumbalo kwa Niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Dkt. Linda Salekwa amewataka wakopaji kuichukua fedha hiyo na kuirejesha kwa wakati ili wananchi wengine waweze kukopa.
“ Mnapewa mikopo hii kumbukeni haina riba, msiende kujengea nyumba fanyeni biashara inayowaingizia kipato ili muweze kurejesha, Mheshimiwa Rais lengo lake ni kuinua wananchi kiuchumi hivyo msimuangushe, chukueni na mrejeshe kwa wakati “
Akizungumza Mkurugenzi wa Halmashauri wa Mji Mafinga Bi Happiness Laizer amewaomba wanavikundi kuwa waadilifu na waaminifu katika urejeshaji wa Mikopo hiyo .
“ wanavikundi walioomba Ni wengi zaidi ya vikundi 62 lakini vikundi vilivyopewa mikopo ni 33 tu, msifanye udanganyifu kwenye pesa hizi msije mkaishia kwenye mikono ya sheria”
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mheshimiwa Regnant Kivinge amesema kuwa Mikopo sio zawadi hivyo lazima irejeshwe ili wengine wakope. Amesema Serikali ya awamu ya Sita ina lengo la kupunguza umaskini kwa wananchi Wake na kuinua uchumi wao kwa kuwapa mitaji.
Vikundi vilivyopewa mikopo ni 33, ambapo wanawake vikundi 19, Vijana vikundi 11 na watu wenye ulemavu vikundi 3 ambapo wanawake wamekopeshwa Tsh. 160,885,505.00 Vijana Tsh. 151,468,123.89.00 na Watu wenye Ulemavu Tsh, 27,800,000.
Wanavikundi hao wamemshukuru Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuanziasha utaratibu huu wa Mikopo isiyo na riba kwani wamedai walio wengi hawanasifa za kukopesheka kwenye taasisi za kifedha hivyo mikopo ya Halmashauri Ni tegemeo kubwa la wananchi kwenye vikundi.
Hafla hiyo imehudhuriwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri, Kamanda wa TAKUKURU Wilaya ya Mufindi, Wakuu wa Idara na wananchi mbalimbali kwenye Makao Makuu ya Halmashauri Luganga.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini- Mafinga Tc
Christopher Mhina
Mwandishi wa Habari- Mafinga TC
@halimadendego
@salekwalinda
@ortamisemi
@maelezonews
Ofisi ya Rais - Tamisemi
Angela Kairuki
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.