• Malalamiko |
    • Wasiliana na sisi |
    • Maswali |
    • Baruapepe |
Mafinga Town Council
Mafinga Town Council

Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Mafinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Organization Structure
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Kilimo na umwagiliaji
      • Fedha
      • Mipango na Takwimu
      • Elimu ya Sekondari
      • Elimu ya Msingi
      • Afya
      • Ardhi na Maliasili
      • Community Development,Social welfare Gender and Youth
      • Water
      • Work
    • Vitengo
      • Community
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Huduma za Kisheria
      • Biashara
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa madiwani
    • Kamati Za Kudumu Za Halmashauri
      • Fedha Na uongozi
      • Mipangomiji Namazingira
      • Uchumi, Fedha Na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana Na Mwenyekiti
  • Miradi Mbalimbali
    • Progressive projects
    • Itakayo Tekelezwa
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Machapisho ya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Makitaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Malalamiko

HALMASHAURI YA MJI WA MAFINGA KUCHANGIA ASILIMIA 10 YA KWA AJILI YA MFUKO WA WANAWAKE ,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAMAVU

Posted on: May 23rd, 2019

Mkuu wa mkoa wa Iringa, Ally Hapi ameiagiza Halmashauri ya Mji Mafinga kuhakikisha wanatenga na kuchangia asilimia 10 ya fedha zinazotokana na mapato ya ndani kwa ajili ya Mfuko wa Wanawake ,Vijana na watu wenye Ulemamavu.

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa, Kaimu Katibu tawala wa mkoa wa Iringa, Lucas Kambelenje wakati wa kikao maalum cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo, alisema kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 37A(1) cha Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa (marekebisho 2018) sura ya 290, suala la kuchangia asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili ya kukopesha vikundi vya Wanawake, vijana na Watu wenye ulemavu vilivyosajiliwa ni la Kisheria kuanzia Julai, 2018.

Alisema kuwa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Mwaka 2017/2018, inaonesha kuwa, Halmashauri ya Mji Mafinga ilichangia kwenye Mfuko huo ,kiasi cha shilingi milioni 90,000,000 tu badala ya shilingi 250,088,994 zilizopaswa kutolewa kutokana na kiasi cha shilingi 2,500,889,940 zilizokusanywa kama mapato ya ndani ya Halmashauri. Hivyo, halmashauri ilishindwa kuchangia shilingi 160,088,994 katika Mfuko wa Wanawake na Vijana

Kambelenje alisema kuwa matumaini serikali  kwa halmashauri hiyo ni kutumia ushirikiano mzuri uliopo kuhakikisha kuwa, hoja zote za ukaguzi zilizotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na zile za Mkaguzi ndani, zinashughulikiwa ipasavyo, ili ziweze kuhakikiwa na kufungwa kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na maelekezo ya Serikali.

“Naamini kuwa, mafanikio haya mazuri yametokana na uwepo wa ushirikiano Mzuri baina yenu Waheshimiwa Madiwani, Watendaji na Wadau mbalimbali wa Halmashauri. Wito wangu kwenu ni kuwa, muendelee kudumisha ushirikiano huu, ili Halmashauri iendelee kupata Hati Safi katika kaguzi zote kila mwaka na pia kuendelea kutoa huduma bora kwa Wananchi wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga.

Aidha alisema kuwa licha ya hoja ya kutenga fedha kwa ajili ya wanawake, vijana na walemavu kwa mujibu wa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Hesabu zilizoishia tarehe 30 Juni, 2018, Halmashauri ya mji Mafinga ina jumla ya hoja 38 ambazo zinatakiwa kufanyiwa kazi.

Aidha alitoa wito kwa Halmashauri iweze kuwa na mifumo bora na imara udhibiti wa ndani, itakayosaidia kulinda na kusimamia ipasavyo matumizi sahihi ya rasilimali na mapato ya Halmashauri, naiagiza Halmashauri ihakikishe kuwa, inakiimarisha kitengo chake Ukaguzi wa ndani kwa kukiwezesha kuwa na wataalam  kutosha na vitendea kazi vya kutosha ili kiweze kutekele majukumu yake ipasavyo kwa wakati na ukamilifu unaostahili

Aliitaka halmashauri ihakikishe kuwa, inasimamia mali zote kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo mbalimbali iliyopo ikiwa kwa kwa mujibu wa agizo la 45(1) la Memoranda ya Fedha za Serikali la Mitaa ya Mwaka 2009 ambayo inaeleza kuwa kuwa, Mali zote ambazo hazitumiki hususan zilizochakaa zitambuliwe na kuwasilishwa kwenye Kamati ya Fedha pamoja na Baraza la Madiwani kwa ajili ya kupata idhini ya kutumwa Wizara ya Fedha ili kuundiwa Bodi ya kuvikagua kwa hatua ya kuvifuta na kuviondosha kama kanuni ya 254 ya kanuni za fedha za mwaka 2001 inavyoelekeza.

Kambelenje aliongeza kuwa halmashauri ihakikishe kuwa, inaweka utaratibu wa kulipa madeni yanayofikia kiasi cha shilingi milioni 510,042,225 ambayo yametokana na madai ya wakandarasi, watoa huduma mbalimbali na watumishi kama ilivyobainishwa katika taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya mwaka 2017/2018.

“Naagiza kuwa, madeni yote yanayostahili kulipwa na fedha za makusanyo ya ndani yahakikiwe na yalipwe mara moja na yale yanayostahili kulipwa na Serikali Kuu, Halmashauri ifanye ufuatiliaji kuhakikisha fedha hizo zinatolewa na kulipwa”” alisema

Aidha, alitoa wito kwa Halmashauri kuacha kulimbikiza au kuongeza madeni hivyo ni vema malipo ya huduma zinazotolewa kwenye  Halmashauri ihakikishe kuwa fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo zinatumika baada ya kupata idhini ya kamati ya Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo.

Akizungumzia hoja hizo makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Mafinga Mh. Zacharia Vang’ota alisema kuwa watahakikisha hoja zote zinafanyiwa kazi ili kusijitokeze hoja nyingine au kuongezeka kwa madeni ambayo halmashauri inadaiwa.

Matangazo

  • NAFASI ZA MASOMO KWA SHULE YA CHIEF MKWAWA ENGLISH MEDIUM- HALMASHAURI YA MJI MAFINGA. NAFASI BADO ZIPO TUPIGIE January 29, 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA YANAPATIKANA www.mafingatc.go.tz July 13, 2024
  • MJI MAFINGA YAVUKA LENGO UKUSANYAJI MAPATO YAKUSANYA ASILIMIA 113 KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024 August 14, 2024
  • MATOKEO YA DARASAM LA SABA 2024 YANAPATIKANA KWENYE TOVUTI YETU .www.mafingatc.go.tz October 30, 2024
  • View All

Habari mpya

  • TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI IMEENDESHA MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA KWA AWAMU YA PILI JIMBO LA MAFINGA MJINI

    May 02, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 KATIKA HALMASHAURI YA MJI MAFINGA UMEPITIA JUMLA YA MIRADI 11 YA MAENDELEO YENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 3.1

    May 01, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 KATIKA HALMASHAURI YA MJI MAFINGA UMEPITIA JUMLA YA MIRADI 11 YA MAENDELEO YENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 3.1

    May 01, 2025
  • MBUNGE WA MAFINGA MJI AKABIDHI MITUNGI YA GESI

    May 01, 2025
  • View All

Video

SENSA NI MAENDELEO
Video zaidi

Viungo Vya Haraka

  • Maelezo na Form Ya kiapo cha uadilifu
  • https://matokeo.necta.go.tz
  • Muongozo wa matumizi ya TEHAMA serikalini

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya wananchi

Watembeleaji kidunia

world map hits counter

Idadi ya watu wanao tembelea Tovuti

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana na sisi

    Mafinga Town.

    Postal Address: Po.Box 76 Mafinga

    Simu: +255 262 772 393

    Mobile: 026-2772393

    Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.