UZINDUZI WA JUKWAA LA WANAWAKE HALMASHAURI YA MAFINGA MJI
Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Mufindi katika uzinduzi wa jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi, lililofanyika mapema hivikaribuni katika Halmashauri ya Mji wa Mafinga,kaimu katibu tawala wa Halmashauri ya Mufindi Joseph Mchina,alisema kuwa jukwaa hilo litaweza kuwasaidia wanawake wilayani humo ili waweze kuondokana hali duni kimaisha.Mchina alisema Katika kusaidia kufikia malengo ya maendeleo endelevu, inaasisitiza uwezeshaji wa wanawake kiuchumi,hivyo wanawake wanatakiwa kujishughulisha katika shughuli mbalimbali ili waweze kujiingizia kipato na hatimae kujikwamua kiuchumi.
Akitoa hotuba yake alisema Majukwaa haya yatasaidia kuongeza uelewa wa wanawake katika uchumi,biashara, upatikanaji wa mitaji, sheria za nchi katika masuala ya uchumi na jinsi ya kujitegemea kiuchumi.Alisema kuwa Lengo la jukwaa la kuwawezesha wanawake kiuchumi ni kukutana na wanawake na kujadiliana kuchangamkia fursa mbalimbali , kuangalia changamoto zinazowakabili na jinsi ya kushiriki kikamilifu katika biashara na shughuli zingine za kiuchumi ili kuwainua "' Naomba kupitia Jukwaa hili la Halmashauri ya Mji wa Mafinga kumpongeza sana Mheshimiwa makamu wa Rais kwa kuteuliwa kwake kuwa mmoja wa Wajumbe wa Timu hii muhimu ya Umoja wa Mataifa ya kuongeza ushiriki wa Wanawake katika shughuli za kiuchumi Duniani. Ili kujenga uelewa wa namna ya kuanzisha majukwaa katika ngazi ya Halmashauri nimeona ni vyema kuzindua jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi ngazi ya Mkoa ili kila Mkurugenzi akaanzishe chombo hiki katika Halmashauri yake kwa kufuata kanuni zilizowekwa’’’alisema Mchina.Aidha aliongeza kuwa Halmashauri ya Mji wa Mafinga kwa kupitia jukwaa la uwezeshaji wanawawke kiuchumi, itahakikisha wanawake wanaondokana na dhana ya kuwa tegemezi,kwa kuhakikisha wanajishughulisha na biashara mbalimbali ili kuondokana na umasikini.
Akitoa Elimu juu ya Ulipaji kodi, Afisa Elimu na Huduma kwa walipa kodi kutoka mamlaka ya mapato Tanzania [TRA] Noveatus Albet alisema kodi ni tozo ya lazima ambayo mtu anawajibika kulipa serikalini kwa mujibu wa sharia ili kuiwezesha serikali kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo ya kijamii.
Albet alisema mfanyabiashara pamoja na kusajiliwa na TRA ana wajibu wa kutunza kumbukumbu za biashara yake,pia iwapo mfanyabiashara ana mauzo yanayoanzia shilingi million 14 na kuendelea kwa mwaka atatakiwa kununua na kutumia mashine za kielektroniki kwa ajili ya kutolea risiti [EFD] Monika Kikoti ni mmoja wa wanawawake walioshiriki maadhimisho hayo , nae alisema kuwa kupitia jukwaa hilo wanawake wataweza kupiga hatua kimaendeleo kwa kujishughulisha na kazi mbalimbali,hali itakayosaidia kuondokana na vitendo vya kunyanyasika na wanaume.
Jumla ya Wanawake 500 kutoka katika kata 9 za Halmashauri hiyo walishiriki uzinduzi huo huo,huku wakiishukuru serikali kwa kutoa kipaumbele kuwawezesha.
MWISHO
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.