Timu ya Wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi wakiongozwa na Mkurugenzi Bwana Afraha Hassan wametembelea Halmashauri ya Mji Mafinga lengo ikiwa ni kubadirishana Utaalamu,Kujengeana uwezo na kushauriana na Wataalamu wa Halmashauri ya Mji Mafinga katika masuala mbalimbali ikiwemo usimamizi wa Miradi ya Maendeleo. Katika Kikao hicho wamejadili Miradi mbalimbali inayotekelezwa na Halmashauri ya Mji Mafinga iliyokamilika na ambayo ipo katika hatua za ujenzi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi Fidelica Myovela amewapongeza Wataalamu kutoka Halmashauri ya Nkasi kwa ziara hii kwani inasaidia kujengeana uwezo katika masuala mbalimbali yanayohusu Miradi ya Maendeleo.
Na,
Anna Mdehwa,
Afisa Habari.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.