Mkurugenzi Bi, Fidelica Myovela akiwa ameambatana na timu ya wakuu wa Idara na Vitengo wametembelea
Shughuli ya kuondoa taka na kuchonga Barabara za kuingia na kutoka eneo la dampo Isalavano

Ambapo Mkurugenzi amepongeza hatua za awali za ukusanyaji taka katika eneo hilo zilipofikia.
Akizungumza Mkurugenzi Bi Myovela amesema "hii ni sehemu ya juhudi za kuimarisha usafi wa mazingira na kuweka mifumo bora ya usimamizi wa taka kwani Dampo hili linahudumia taka zote zinazokusanywa na Halmashauri ya Mji Mafinga hivyo ni vyema miundombinu iwekwe vizuri." Amesema Bi, Fidelica.

Pia amesisitiza umuhimu wa utunzwaji wa dampo ilo kwa kuzingatia viwango vya kitaalamu vya utunzwaji wa mazingira ya dampo.
Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Usafi wa Mazingira Charles Tuyi amesema " Mpaka hapa tulipofikia ni hatua kubwa ninauhakika lengo tuliojiwekea litatimia la kuzuia taka zisitapakae eneo la Dampo na hivyo itatusaidia kuzuia magonjwa ya mlipuko." Amesema Tuyi
Pia katika ziara hiyo wametembelea ujenzi wa Shule ya Msingi JJ Mungai pamoja na Ujenzi wa vyumba vinne vya Madarasa Shule ya Msingi Lumwago na wodi ya Wazazi kituo cha Afya Upendo.
Mkurugenzi Bi. Myovela amewataka wasimamizi wa Shughuli na Miradi hiyo kuhakikisha wanazingatia viwango vya ubora vilivyowekwa na kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa wakati.
Na
Anna Mdehwa
Afisa Habari.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.