Shule ya sekondari changarawe yatoa motisha ya shilingi 8,040,000 kwa walimu walio faulisha vizuri katika masomo mbalimbali .
Akitoa zawadi hizo kwa walimu Afisa Elimu Idara ya Sekondari Halmashauri ya Mji Mafinga Stephen Shemdoe amesema ameupongeza uongozi wa shule ya sekondari Changarawe kwa kutoa motisha ni jambo la msingi na lenye tija kwani imekuwa iwasaida mwalimu kufanya vizuri katika kazi zao ikiwemo kufundisha kwa weledi mkubwa na kuwa karibu na wanafunzi wao napia kuwatia moyo.
Pia amewataka walimu kuendeleza ushirikiano na uwongozi pamoja na wanafunzi ili kuhakikisha shule inaenda mbele katika taaluma na nidhamu hii itasaidia kuzalisha wanafunzi wenye weledi na maono huko mbele na kulisaidia taifa .
Aidha Afisa Elimu Stephen Shemdoe amewapongeza walimu wote pamoja na uwongozi wa shule ya sekondari changarawe kwa kuendelea kusimamia miradi ya elimu ambayo inaletwa kwani kufanya hivyo ni uzalendo mkubwa na hii itasaidia kukuza elimu katika eneo hili la Changarawe.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Changarawe Peter Mbata amemshukuru Afisa Elimu Sekondari kwa kuendelea kutatua kero mbalimbali ikiwemo kupeleka walimu kwa wakati napia kusikiliza kero za walimu na kuzitatua haraka pia ameongeza kwa kusema Shule ya Sekondari Changarawe itaendelea kutoa motisha kwa kiwango kikubwa zaidi kwa walimu ambao wanafanya vizuri na pia kwa wafanyakazi wengine ambao wapo hapa lengo ikiwa ni kusamini mchango wao katika shule
Michael Ngowi Afisa Habari.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.