Jumla ya washiriki 92 kutoka katika viwanda 19 vinavyozalisha, kuchakata na kuuza nguzo za Miti zinazosambaza Nishati ya Umeme hapa Nchini kutoka katika mikoa minne wamepatiwa mafunzo maalumu kutoka Shirika la Viwango Tanzania( TBS)ya kuhakikisha kuwa miti inayolimwa, inachakatwa na kuuzwa inakidhi matakwa ya viwango ili kuweza kukuza wigo wa masoko na kuongeza pato la Taifa.
Akizungumza Katibu Tawala Wilaya ya Mufindi Ndugu, Frank Sichalwe kwaniaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Dkt. Linda Salekwa amesema mafunzo haya ni mapendekezo ya Kamati Maalumu ya kushauri namna ya kudhibiti ubora wa nguzo za Miti.
Amesema katika mafunzo haya TBS imeshirikisha taasisi nyingine za Serikali ikiwemo TANESCO, REA na TFS lengo likiwa nikutoa elimu kwa wazalishaji wa nguzo za miti zinazotumika kusambaza nishati ya Umeme.
DAS Sichalwe amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha wazalishaji wa nguzo hapa nchini wanazalisha nguzo bora na kufikia Soko la Nje ili kuweza kuongeza pato la nchi na la watanzania kwa ujumla.
Nae Meneja wa Shirika la Viwango Tanzania Kanda ya nyanda za Juu Kusini Ndugu, Abel Mwakasonda amesema Moja ya majukumu ya TBS kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Viwango sura Na. 130 kifungu cha 4(1) (h) ni kutoa elimu kwa wadau wa vuwandani na kwenye sekta za huduma kuhusu maswala ya viwango, ubora, upimaji, usalama wa chakula na vipodozi na majengo yanayotumika kuzalishia na kuuzia bidhaa hizo.
Ameongeza kuwa mafunzo haya kutoka TBS yanafundisha namna bora kudhibiti ubora wa nguzo za miti kama ilivyo azma ya Serikali.
Nae Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazalishaji nguzo Tanzania (TAWPA) Ndugu, Kikolo Mwakasungula amesema mafunzo haya kutoka TBS yamehudhuriwa na washiriki kutoka Iringa, Njombe, Kigoma, Tanga na Mara na kuogeza kuwa mafunzo yatasaidia wazalishaji kuzalisha nguzo bora zinazokidhi ubora wa ndani na nje ya nchi.
Mafunzo haya yamehudhuriwa na Wakurugenzi wa Wilaya ya Mufindi akiwemo Mkurugenzi wa Mji Mafingw Ndugu. Ayoub Kambi na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Ndugu Fussi na viongozi kutoka TBS.
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano-mafinga TC
Sima Bingileki
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Mafinga TC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.