Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Ndugu Charles Mwaitege ameendesha kikao cha Kamati ya Lishe kujadili taarifa mbalimbali kwa robo ya tatu kuanzia mwezi Januari hadi Machi 2025.
Katika kikao hicho Kaimu Mkurugenzi Ndugu Charles Mwaitege amezitaka Idara za elimu Msingi na Sekondari kuhakikisha wanazalisha mazao ya chakula kama mahindi ,maharage,na viazi ili kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula pindi wanapokuwepo shuleni.
Aidha amesisitiza kuendelea kutoa elimu kwa wazazi na walezi kuhakikisha wanachangia chakula shuleni ili kuweza kuongeza ufaulu na kupunguza utoro pia kuhakikisha walimu wote wanasimamia zoezi hili kwa ukaribu zaidi.
Pia amewataka Maafisa Afya kuendelea kutoa elimu ya afya kwa makundi na wananchi mbalimbali juu ya matumizi bora ya lishe na matumizi sahihii ya bidhaa mbalimbali ili kuepuka kutengeneza sumu mbalimbali zitokanazo na bidhaa tunazo tumia.
Michael Ngowi
Afisa Habari
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.