Kamati ya Elimu, Afya na Uchumi ya Halmashauri ya Mji Mafinga ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Monica Luvanda imekagua utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ya ujenzi wa vyumba 4 vya madarasa, Mabweni 2, matundu 10 ya vyoo kwa ajili ya kidato cha tano shule ya Secondari Ndolezi mradi unaoendelea kupitia fedha ya Serikali kuu wenye thamani ya milioni 380,000,000. Pamoja na ujenzi wa nyumba ya Walimu Two in one wenye thamani ya milioni 100,000,000 kupitia Mradi wa SEQUIP.
''Nawapongeza sana kwa muda ambao umetumika katika kutekeleza Miradi hii kwani kwa muda mfupi imefikia hatua inayoridhisha naomba Miradi ikamilike kwa muda uliopangwa" Maneno hayo yamesemwa na Mheshimiwa Diwani Monica Luvanda baada ya kutembelea miradi yote iyo.
Kamati pia wametembelea ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa na matundu 6 ya vyoo shule ya Msingi Ifingo Mradi wenye thamani ya Milioni 63,000,000 BOOST II katika Kata ya Kinyanambo.
Katika Kata ya Upendo wamekagua shule Mpya ya Secondari Upendo shule inayojengwa kupitia Mradi wa SEQUIP wenye thamani ya Milioni 583,180,028 ambapo Miradi yote ipo katika hatua za utekelezaji ambapo majengo yote yanatarajiwa Kuanza kutumika mapema mwaka ujao.
Ziara imehudhuliwa na Wajumbe wa Kamati Waheshimiwa Madiwani pamoja na baadhi ya Wataalam wa Halmashauri ya Mafinga Mji ambapo wamefanya ziara katika kata tatu ambazo ni Boma, Kinyanambo na Upendo.
Imetolewa na kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Mafinga Tc
Anna Mdehwa.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.