KAMATI YA ELIMU, AFYA NA UCHUMI YAFANYA ZIARA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO-MAFINGA TC
Kamati ya Elimu Afya na Uchumi inayoongozwa na Mwenyekiti ambaye ni Diwani wa Kata ya Rungemba Mheshimiwa Samweli Mwalongo imefanya ziara kukagua Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa chini ya Kamati hiyo.
Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa ni Mradi wa Ujenzi wa Vyumba Viwili vya Madarasa na Ofisi moja katika Shue ya Msingi Ihumo, Mradi wa Ujenzi wa Chumba Kimoja cha Darasa na Ofisi katika Shule ya Sekondari Isalavanu na Ujenzi unaoendelea katika Kituo cha Afya Bumilayinga.
Aidha, Wajumbe wa Kamati hiyo baada ya Kutembelea waliweza kutoa Mawazo yao kuhusu Miradi hiyo ikiwa ni pamoja Kupongeza Halmashauri kwa Usimamizi mzuri wa Miradi na kushauri halmashauri kukamilisha Miradi iliyobaki kama ya Madarasa katika Shule ya Msingi Ihumo ili wanafuzi waweze kutumia madarasa hayo.
Kaimu Mkurugenzi Ndugu Charles Tuyi aliongoza Wataalamu mbalimbali kutoka Halmashauri kushiriki ziara hiyo.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-MAFINGATC
Sima Bingileki
Afisa Habari Mkuu
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.