KAMATI YA ELIMU, AFYA NA UCHUMI HALMASHAURI YA MJI MAFINGA YATEMBELEA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO- MAFINGA TC.
Kamati ya Elimu, Afya na Uchumi Halmashauri ya Mji Mafinga chini ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Samwel Mwalongoi Diwani wa Kata ya Rungemba imefanya ziara ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa chini ya Kamati hiyo.
Miradi iliyotembelewa na Kamati ni:-
Ujenzi wa Kituo cha Afya Upendo, ambapo linajengwa jengo la Wagonjwa wa Nje (OPD) hatua:- ujenzi unaendelea na fedha zilizopokelewa ni shilingi milioni 150 kutoka serikali kuu na jengo linatarajiwa kukamilia tarehe 19/9/2022.
-Ujenzi wa Kituo cha Afya Ifingo katika kata ya Kinyanambo. Ujenzi wa Jengo la Upasuaji, Jengo la Kufulia na Njia za kuunganisha majengo. Ujenzi huu ni ujenzi wa awamu ya tatu na fedha zilizopokelewa ni shilingi milioni 250 kutoka Serikali Kuu. Ujenzi upo katika hatua za Umaliziaji.
-Ujenzi wa Madarasa Mawili Shule ya Sekondari Upendo. Ujenzi umekamilika na fedha iliyopokelewa ni shilingi milioni 40 kutoka Serikali Kuu.
-Ujenzi wa Choo Soko Jipya la Pipeline unaendelea na Ujenzi wa Mnara wa Tanki la Maji na Ukarabati wa Choo Uwanja wa Mashujaa Ujenzi umekamilika.
-Ujenzi wa Darasa moja Shule ya Sekondari Luganga. Ujenzi huu umekamilika na darasa linatumika ambapo jumla ya fedha zilizopokelewa kutoka Serikali Kuu ni shilingi milioni 20
Waheshimiwa Madiwani wa Kamati hiyo wameipongeza na Kuishukuru Serikali kwa kuendelea kuleta fedha za Maendeleo katika Halmashauri ya Mji Mafinga na Kupongeza Timu ya Menejimenti ikiongozwa na Mkurugenzi Bi Happiness Laizer na watendaji wote wa Halmashauri kwa kazi nzuri ya Usimamizi wa Miradi ya Maendeleo.
“ Miradi ni mizuri sana, thamani ya fedha na miradi vinaendana kwa kweli tuwapongeze kwa kazi nzuri mno ya usimamizi wa Miradi, kikubwa ambacho tunasisitiza ni ukamilishaji miradi hii kwa wakati, tujitahidi miradi ikamilike kwa muda uliopangwa ili kupunguza changamoto kwa jamii ya wananchi wa Mji wa Mafinga na watanzania kwa ujumla hasa kwa wananchi wa maeneo husika.” Kauli ya Mheshimiwa Samwel Mwalongo Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na Uchumi.
IMEANDALIWA NA OFISI YA HABARI NA MAWASILIANO-MAFINGA TC
Sima Bingileki
Afisa Habari Mkuu.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.