Kamati ya Fedha na Utawala ya Halmashauri ya Mji Mafinga ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mheshimiwa Regnant Kivinge imefanya ziara ya kukagua Miradi ya Maendeleo kwa kipindi cha Robo ya kwanza 2024/2025 ambapo imekagua ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na ujenzi wa matundu 6 ya vyoo katika Shule ya Msingi Kilimani Kata ya Isalavanu.
Akitoa taarifa ya Ujenzi wa vyumba hivyo vitatu vya madarasa na Matundu 6 ya vyoo vya wasichana, Mkuu wa Shule ya Kilimani Mwalimu kwaniaba ya Mkurugenzi wa Mji Mafinga Bi Fidelica Myovella amesema tarehe 18/6/2024 Fedha kiasi cha shilingi Milioni 88 kilipokelewa kwaajili ya ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa milioni 75 na Milioni 13 kwaajili ya ujenzi wa Matundu 6 ya vyoo hivyo kufanya jumla ya fedha pokelewa kutoka Serikali Kuu kupitia Mradi wa Boost kuwa milioni 88.
Amesema hatua ya ujenzi iliyofikiwa ni ukamilishaji wa upakaji wa Rangi na jengo la choo lipo hatua ya kupiga lipu.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti waheshimiwa madiwani wa kamati ya Fedha na Utawala wamepongeza hatua iliyofikiwa ya ukamilishaji na kuomba wataalamu kuhakikisha fundi anasimamiwa kwa ukaribu ili akamilishe kazi kwa wakati.
Ziara hiyo imehudhuriwa na Katibu Tawala Wilaya ya Mufindi Ndugu Reuben Chongolo , Kaimu Mkurugenzi Mji Mafinga Ndugu Peter Ngusa, Wakuu wa Idara na Vitengo na Watendaji wa Kata Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini - Mafinga TC
Sima Mark Bingileki
Mkuu wa Kitengo- Mafinga TC
Picha mbalimbali katika ukaguzi wa miradi kwa robo ya kwanza 2024 /2025
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.