Kamati ya Fedha na Utawala ya Halmashauri ya Mji Mafinga inayoongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mheshimiwa Regnant Kivinge akiwa na wajumbe wa Kamati hiyo wamefanya ziara kukagua Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa chini ya Kamati hiyo kwa kipindi cha robo ya Tatu, Januari - Machi 2025.
Akizungumza baada ya kufanya ziara hiyo, Mwenyekiti na wajumbe wamepongeza Timu ya Menejimenti ya Mji Mafinga inayoongozwa na Mkurugenzi wa Mji Bi Fidelica Myovella kwa usimamizi wa moja kwa moja wa Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo na Ufuatiliaji wa karibu kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa wakati na thamani ya Mradi na Fedha vinaendana.
Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa ni Ujenzi wa nyumba ya mtumishi katika Kituo cha Afya Ifingo, jengo la upasuaji kituo cha Afya Upendo, ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa na ofisi Shule ya msingi Itamba, ujenzi wa madarasa mawili shule ya msingi Maarifa na Shule mpya ya Sekondari ya Amali.
Wakuu wa Idara ma wataalamu wengine wamehudhuria ziara hiyo ya Kamati ya Fedha na Uongozi kwa kipindi cha Robo ya Tatu Januari- Machi.
Sima Bingileki
Afisa Habari Mkuu
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.