Mwenyekiti wa Kamati Mhe, Monica Luvanda akiwa ameongozana na Waheshimiwa, Madiwani Meja Kalinga, Denis Kutemile ambao ni Wajumbe wa Kamati pamoja na Wataalamu kutoka Halmashauri ya Mji Mafinga wametembelea Miradi minne ya Maendeleo ili kukagua ambayo ni :-
Ujenzi nyumba ya Watumishi( Two in One) wa Afya Ifingo Mradi unaogharimu fedha za Kitanzania Milioni 90 Fedha zinazotokana na Mapato ya ndani na mpaka sasa imetumika 53,953,899.51 na upo katika hatua ya kusawazisha ukuta.
Shule ya Msingi Amani ( Bweni na Jiko) ambapo kwa bweni limekamilika na limegharimu kiasi cha 80,000,000/= chanzo cha mapato Serikali Kuu. Na Jiko ambalo mpaka kukamilika inatarajiwa kutumika 38,131,040/= Chanzo cha Mapato ni Halmashauri ya Mji Mafinga Mapato ya ndani.
Ujenzi wa njia za kutembelea katika Hospitali ya Mji Mafinga ambao umegharimu 84,824,360/= na Tayari umekamilika Mradi ambao fedha inatokana na zilizobaki baada ya kukamilisha ujenzi wa Miundombinu kupitia fedha kutoka Serikali Kuu.
Shule ya Sekondari ya Amali Changarawe ni Mradi ambao unatekelezwa kwa fedha kutoka Serikali Kuu ambapo mpaka kukamilika unatarajiwa kugharimu Bilioni 1 na Milioni Mia sita ambapo majengo 19 tayali yameshajengwa ikiwemo madarasa 8, mabweni 2, na Maktaba.
“Kwakweli niwapongeze sana kwa hatua ambayo Miradi imefikia kwa usimamizi Mzuri wa Wataalamu wa Halmashauri ya Mji Mafinga pamoja na Serikali kwa kutupatia Fedha na Wananchi kwa ujumla wanaozunguka maeneo ya Mradi kwa nguvu kazi wanayoitoa katika Miradi ya Maendeleo.Amesema Mwenyekiti wa Kamati Monica Luvanda.
Pia wajumbe walipongeza hasa kwenye kasi ya ujenzi, thamani, ya fedha na ubora wa Miradi.
Na,
Anna Mdehwa,
Afisa Habari.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.