Kamati ya UKIMWI ya Halmashauri ya Mji Mafinga ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Samweli Mwalongo imefanya ziara ya kukagua na kuangalia huduma za (CTC) zinazotolewa katika Zahanati ya Rungemba ikiwa ni kudhibiti maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Mganga Mfawidhi wa zahanati ya Rungemba Ndugu Isdori Luteganisia ameiambia Kamati hiyo kuwa wapokea hudumu wanaendelea kufuata maelekezo ya watalaamu pamoja na wadau wa afya wanayopewa ikiwemo kuchukua dawa kwa wakati, kufanya vipimo mara kwa mara ili kuangalia mwenenendo wa afya zao.
Pia amesema kuwa Zahanati ya Rungemba imeendelea kutoa huduma bila kupata malalamiko kutoka kwa wapokea huduma na wataendelea kutoa elimu kwa kushirikiana na wadau wa Afya ili kuweza kuwafikia wapata huduma kwa urahisi katika ngazi ya jamii.
Aidha Mwenyekiti ya Kamati ya Ukimwi Mheshimiwa Samweli Mwalongo amewapongeza Madaktari na watoa huduma, pamoja na wadau mbalimbali kwa kazi kubwa ambayo wanaifanya katika jamii hivyo ametoa rai kwa wadau kuendelea kushirikiana na Serikali ili kuhakikisha wapata huduma wote wanafikiwa na kupewa elimu.
Picha mbalimbali za Wajumbe wa Kamati ya Ukimwi wakiwa wametembelea Zahanati ya Rungemba kuangalia utoaji wa huduma za CTC.
Michael Ngowi
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.