Diwani wa Kata ya Isalavanu Mheshimiwa Charles Makoga ameongoza Kamati ya Mipango miji kuangalia nakukagua miradi ya miundombinu katika Halmashauri ya Mji Mafinga.
Kamati hiyo imekagua barabara katika eneo la Luganga yenye jumla ya kilometa 35 ambazo zimechongwa katika mitaa hiyo ambapo jumla ya shilingi milioni 46 zimepangwa kutumika katika mwaka huu wa fedha.
Pia Kamati hiyo imetembelea eneo la Makalala lenye ukubwa wa hekta 567.81 ambalo litatumika kwa shughuli za maziko sambamba na hilo pia kamati imekagua barabara ya mzunguko iliyojengwa kwa kiwango cha changarawe na pia inatarajiwa kuzinduliwa na mwenge wa Uhuru hivi karibuni.
Aidha Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Charles Makoga amepongeza timu ya wataalamu kutoka Halmashauri kwa kuendelea kusimamia miradi ambayo imekuwa ikiibuliwa na lengo ni kuhakikisha tunawasaidia wananchi wetu kupata huduma bora.
Michael Ngowi
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.