Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa imefanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya Mji Mafinga.
Kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Ndugu Daudi Yassin pamoja na Mkuu wa Mkoa Mheshimiwa Piter Serukamba na wajumbe wengine wamekagua mradi wa Shule ya Amali ambao unatekelezwa na fedha kutoka Serikali kuu jumla ya kiasi cha shilingi bilioni moja na milioni mia sita (1.6B) ambapo ujenzi huo umefikia asilimia 95 ya utekelezaji ikijumuisha mindombinu mbalimbali.
Aidha Kamati ya Siasa ya Mkoa imepitia na kukagua ujenzi wa mradi wa Maji wa Miji 28 ambao unatekelezwa kwa kiasi cha fedha shilingi bilioni 48 ambapo ujenzi umefikia asilimia 20 hata hivyo Kamati ya Siasa imemtaka mkandarasi kuhakikisha anaendana na kasi ili kukamilisha mradi huo kwa wakati ambao utapunguza nakumaliza shida ya maji katika Mji wa Mafinga.
Pia Kamati ya Siasa emekagua mradi wa uboreshaji wa hospitali ya Mji Mafinga ambapo ujenzi huo unajumuisha jengo la wazazi, jengo la kufulia, jengo la kuhudumia wagonjwa mahututi (ICU) na ujenzi wa walkway mradi huu unatekelezwa kwa fedha kutoka serikali kuu jumla ya kiasi cha shilingi milioni mia tisa (900,000,000) ambapo mradi huu upo katika hatua za umaliziaji ili uwanze kutoa huduma kwa wananchi.
Kwaupande mwingine Kamati ya Siasa ya Mkoa kupitia kwa Mwenyekiti wake Ndugu Daudi Yassin amepongeza jitihada zinazofanywa na Serikali katika kusimamia miradi hii kwa ukamilifu mkubwa kwani itenda kutatua kero kwa watu wetu na kuwapa huduma bora na pia amepongeza usimamiaji wa fedha zote ambazo zinaletwa na Serikali kwaajili ya utekelezaji wa Ilani .
Pia ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwaajili ya miradi mbalimbali katika Halmashauri ya Mji Mafinga ambayo inachochea ukuaji na utoaji wa huduma bora kwa wananchi .
Michael Ngowi
Afisa Habari
Picha mbalimbali za ziara ya Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapindunzi Mkoa wa Iringa katika Halmashauri ya Mji Mafinga ikikagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.