Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Mufindi ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa George Kavenuke imefanya ziara ya kukagua na kutoa Ushauri kwenye Miradi mbalimbali itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru tarehe 5/5/2023.
Miradi hiyo ni:-
-Kiwanda cha Lush Chanzo, -Ujenzi wa Tenki la Maji
-Chuo cha FWITC PandaMiti Kibiashara
-Ujenzi wa Maabara Upendo Sekondari
-Ujenzi wa Barabara Mtaa wa Mkombwe
-Uendelezaji wa Vikundi vya Vijana
-Ujenzi wa Kituo cha Mafuta NFS Mafinga
-Ujenzi wa Jengo la EMD
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Mufindi ni Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Dkt. Linda Salekwa , Katibu wa CCM Wilaya ya Mufindi Frida Kaaya pamoja na Waheshimiwa wa Halmashauri ya Mji Mafinga na Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi.
Kamati hiyo imeambatana na Mkurugenzi wa Mji Mafinga Bi, Happiness Laizer na Wataalamu wa Halmashauri ya Mji Mafinga.
Mwenge wa Uhuru 2023 Unatarajiwa kukimbizwa Halmashauri ya Mji Mafinga tarehe 5/5/2023 na unatarajiwa kukesha katika Uwanja wa Mashujaa na utakabidhiwa mkoa wa Morogoro tarehe 6/5/2023
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI- MAFINGA TC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.