KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOA WA IRINGA IKIONGOZWA NA MKUU WA MKOA WA IRINGA MHE. HALIMA DENDEGO IMEFANYA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI PENDEKEZWA ITAKAYO PITIWA NA MWENGE WA UHURU TAREHE 5/5/2023 KATIKA HALMASHAURI YA MJI MAFINGA.
Akikagua Miradi hiyo Mkuu wa Mkoa wa Iringa akiwa ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa pamoja Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Mufindi ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Dkt. Linda Linda Salejwa amesema Miradi iliyopendekezwa yote inagusa maslahi ya wananchi na Mingi imekamilika Aidha kwa Miradi yenye marekebisho ameagiza yafanyike mapema ili Mwenge wa Uhuru utakague, kuweka jiwe la Msingi na Kuzindua Miradi hiyo.
Miradi pendekezwa iliyotembelewa ni:-
- Kuweka Jiwe la Msingi Kiwanda cha Lush Chanzo kinachohusika na uzalishaji wa MDF BOARD
- Uzinduzi wa Mradi wa Maji Makwawa.
- Uzinduzi wa Kitalu cha miche ya Kisasa ya Miti - PandaMiti Kibiashara.
- Kuzindua Ujenzi wa Maabara katika Shule ya Sekondari Upendo
- Kuweka Jiwe la Msingi ujenzi wa barabara Mtaa wa Mkombwe.
- Kukagua vikundi vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu Kata ya Boma.
- Uzinduzi wa Kituo cha Mafuta NFS Kata ya Changarawe
- Uzinduzi ww Jengo la huduma za dharura(EMD)
Katika Halmashauri ya Mji Mafinga Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kupokelewa tarehe 5/5/2023 na utakesha katika Uwanja wa Mashujaa ambapo tarehe 6/5/2023 mwenge wa Uhuru utakabidhiwa Mkoani Morogoro.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI- MAFINGA TC
Sima Bingileki
Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.