Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Mufindi ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Saad Mtambule imefanya zira kukagua miradi pendekezwa itakayo pitiwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru Tarehe 6/9/2022 katika Halmashauri ya Mji Mafinga.
Miradi iliyopitiwa na Kamati hiyo ya Ulinzi na Usalama Wilaya ni pamoja na
Ujenzi wa Bweni katika Shule ya Msingi Amani- Kuzindua
Ujenzi wa Kisima cha Maji( Water for Africa)-Kuzindua
Mradi wa kuotesha miche ya parachichi- Kukagua
NESA vacational training centre- Kukagua
Mradi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami-Kuzindua
Ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na ofisi moja Changarawe Sekondari- Kuzindua
Ujenzi wa jengo la kutoa huduma za dharula(EMD) Mafinga Hospitali.
Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Mji Mafinga unatarajiwa kupokewa katika viwanja vya Shule ya Msingi Amani na unatarajiwa kukesha katika Uwanja wa Mashujaa.
Timu ya wataalamu katika ziara hiyo iliongozwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi, Happiness Laizer.
IMEANDALIWA NA
OFISI YA HABARI NA MAWASILIANO-MAFINGA TC.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.