Kamati ya Usalama Mkoa wa Iringa ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Peter Serukamba imefanya ziara kukagua njia na Miradi itakayo zinduliwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru Mei 1, 2025 katika Halmashauri ya Mji Mafinga.
Akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Peter Serukamba amesema Miradi iliyopendekezwa ni Mizuri na mingine inahitaji nguvu ili ikamilike kabla ya mwenge kupita.
“ Hakikisheni Miradi hii inakamilika mapema kabla yq Mwenge kupita, nyarakq zote ziwepo zinazohitajika na kasoro ndogo ndogo hakikisheni mnazitatua mapema, muda uliosalia sio mkubwa tuhakikishe kwenye Miradi yote taarifa zote zipo zinazohitajika”
Amesema lengo ni kuhakikisha Miradi ya Wananchi inakamilika kwa wakati ili kuongeza Tija kwa wananchi na kuendelea kushikilia nafasi ya kwanza kwa Mji Mafinga Kitaifa kwenye kanda ya pili na nafasi ya Kwanza Kimkoa.
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa kapitia njia ya Mwenge na Miradi Ifuatayo:-
Mradi ya nyumba 2 in 1 katika Kituo Cha Afya Ifingo.
Mradi wa Ujenzi wa Bweni la watoto wenye uhitaji maalumu Katika Shule ya Msingi Amani
Mradi wa Maji
Mradi wa Ujenzi wa Madarasa. Mawili- Shule ya
Msingi Amani na Mradi wa Kuendeleza vijana
Ziara hiyo imehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Dkt. Linda Salekwa na Kamati ya Usalama Wilaya pamoja na Mkurugenzi wa Mji Mafinga Bi. Fidelica Myovella akiwa na Wajumbe wa Timu ya Menejimenti na Mratibu wa Mwenge Mkoa na Wilaya.
Sima Bingileki
Afisa Habari Mkuu
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.