Kila Maendeleo yanayofanyika kwenye Mamlaka yoyote au Taasisi lazima vikaliwe vikao vya majadiliano kujadili mustakabali wa Eneo husika katika nyanja mbalimbali lengo likiwa ni kutafuta njia ya kusonga mbele na kutatua changamoto zilizopo.
Hii imedhihirishwa leo tarehe 14/4/2025 ambapo kimefanyika kikao cha Kujadili Maendeleo ya Kata (KAMAKA) katika Kata ya Isalavanu kikao kilichofanyika katika Shule ya Sekondari Isalavanu.
Kikao hicho kimeongozwa ma Mwenyekiti ambaye ni Diwani wa Kata ya Isalavanu Mheshimiwa Charles John Makoga na Katibu akiwa ni Mtendaji wa Katq Ndugu Nuru Mande na kimehudhuriwa na wajumbe mbalimbali kutoka Ngazi ya Kata na Mitaa.
Katika kikao hicho agenda zilizo jadiliwa ni Lishe, Biashara, Kilimo, Ulinzi na Usalama.
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini- Mafinga TC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.