KATIBU TAWALA MKOA WA IRINGA AFUNGUA MAFUNZO KWA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII-MAFINGA TC
Katibu Tawala Mkoa wa Iringa Bi, Happiness Seneda amefungua mafunzo ya mfumo wa usimamizi wa mikopo inayotokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Mji Mafinga.
Amesema mfumo utaanza rasmi kutumika tarehe 1/7/2022 ambapo utarahisisha vikundi vyote kuingizwa kwenye mfumo huo, usimamizi wa marejesho, utoaji w mikopo utakuwa wa haki na hakuna mtu atakopa kwenye vikundi viwili kwa kufanya udanganyifu kwani mfumo utamkataa.
Bi, Seneda ameongeza kuwa lengo la serikali ni kuona wananchi wanaondokana na umaskini na wanaweza kusimamia uchumi wao, hivyo anatarajia mafunzo hayo yalete matokeo chanya na kuondokana na changamoto zilizokuwepo hapo nyuma katika ukopeshwaji, urejeshaji na usimamizi wa mikopo hiyo ya makundi ya Wanawake, Vijana na watu wenye Ulemavu.
Aidha Kuhusu zoezi la Kitaifa la SENSA ya watu na makazi, Katibu Tawala amesema Elimu iendelee kutolewa kwa wananchi ili waweze kushiriki zoezi hilo kikamilifu tarehe 23 Agosti kwani litasaidia kupanga mipango ya Serikali kwa sekta zote.
Mafunzo hayo, yametolewa na wawezeshaji ngazi ya mkoa wa Iringa na kuhudhuriwa na baadhi ya Wakuu wa Idara pamoja na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Mji Mafinga Ndugu, Charles Tuyi Afisa Mazingira.
IMEANDALIWA NA
OFISI YA HABARI NA MAWASILIANO-MAFINGA TC
Sima Bingileki
Afisa Habari Mkuu
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.