“ Sifa ya Wilaya ya Mufindi inatokana na nyie watumishi kufanya kazi kwa bidii katika Sekta zote, kwa kuweka malengo ya Serikali mbele ya kutoa huduma Bora kwa wananchi na kusimamia Miradi ya Maendeleo “
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Tawala Wilaya ya Mufindi Ndugu Frank Sichalwe alipokuwa Akizungumza na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Mji Mafinga ikiwa ni ziara ya kikazi katika kuwajenga watumishi, kuwakumbusha wajibu wao na kuwapa hari chanya ya kazi Kati kutoa huduma kwa wananchi.
Amesema kila mmoja anatakiwa kutimiza wajibu Wake katika kazi ikiwa ni pamoja na kuheshimu viongozi waliopo, kuheshimu walio chini yenu na kuhakikisha Mapato yanakusanywa na kufikia malengo.
Ndugu Sichalwe Amewahakilishia watumishi wa Wilaya ya Mufindi Ushirikiano wa hali ya juu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Dkt. Linda Salekwa na wakati wowote waitumie Ofisi katika kutaka Ushauri katika Utendaji wa Kazi.
“Hakuna mtu wa Lazima, ila kuna mtu muhimu”
Tujitahidi tuwe muhimu kwenye maeneo yetu ya kazi. Mkumbuke hakuna mtu ambaye Ni lazima awepo, kwani Leo unaweza ukawa haupo na kazi zako akaja mwingine akazifanya, hivyo tuishi kwa kupendana katika maeneo yetu ya kazi na Kwa unyenyekevu mkubwa ili tutimize malengo ya Serikali.”
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Ndugu Ayoub Kambi kwa niaba ya Wakuu wa Divisheni na Vitengo amesema atahakikisha watumishi wanafanya kazi kwa bidii, kujituma bila kumkwamisha kiongozi yeyote na kuhudumia wananchi ili malengo ya Serikali yaweze kufikiwa ya kutoa huduma Bora kwa haraka,kusimamia Fedha za Miradi ya Maendeleo na kukusanya mapato ya Serikali.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-MAFINGA TC
Sima Bingileki
Kaimu Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini- Mafinga Tc
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.