KIFAA CHA UPIMAJI VIWANJA (RTK) CHENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 32 CHANUNULIWA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI HALMASHAURI YA MJI MAFINGA.
“Kifa hiki kina uwezo wa kupima zaidi ya Viwanja 100 kwa siku moja, Kifaa kitasaidia kupunguza Migogoro ya Ardhi, Kufufua Mipaka iliyopotea na kuwa Chanzo cha Mapato cha Halmashauri ya Mji Mafinga”
Akizungumza wakati akitoa ufafanuzi kuhusu jinsi ya kutumia kifaa hicho, Mpima Ardhi, Halmashauri ya Mji Mafinga Rashid Mgambo amesema kifa kinaweza kupima Zaidi ya viwanja 80-100 kwa siku kulingana na matumizi ya mtumaji. Pia kifaa kitapunguza Migogoro ya Ardhi na kufichua Mipaka iliyopotea.
Akikabidhi kifaa hicho kwa Idara ya Ardhi Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Mheshimiwa Regnant Kivinge amesema kuwa hakika ni hatua ya kupongezwa kwa Uongozi wa Mji Mafinga kwa kuamua kununua kifaa hiki kwani kwa kiasi kikubwa kitaleta mabadiliko makubwa kwa Sekta ya Ardhi katika Mji wa Mafinga..
Amempongeza Mkurugenzi wa Mji Mafinga Bi Happiness Laizer na Wataalamu kwa kuona umuhimu wa kumiliki kifaa hicho cha RTK ambacho kitapunguza Migogoro ya Ardhi, Kufichua Mipaka iliyopotea na Kuongeza Mapato ya Halmashauri.
Makabidhiano hayo yamefanyika nje ya Jengo la Halmashauri na kushuhudiwa na Mbunge wa Viti Maalumu Mheshimiwa Rose Tweve, Waheshimiwa Madiwani, Pamoja na Kamati ya Ulinzi ya Wilaya.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI- MAFINGATC
Sima Bingileki
Afisa Habari Mkuu.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.