“Hakikisheni malengo mliyoombea Mradi mnayafikia na takwimu zinakuwa Sahihi kwakuwa Mashirika haya yanatekeleza kwa Umoja Malengo ya Serikali.”
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mji Mafinga Bi. Fidelica Myovella alipokuwa akifungua kikao cha Robo ya Kwanza cha Baraza la Mashirika yasiyo ya Kiserikali kilichofanyika tarehe 1/10/2024 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji Mafinga na kuhudhuriwa na Wawakishi kutoka Mashirika Mbalimbali ngazi ya Wilaya”
“Mashirika yasiyo ya kiserikali yanaunga mkono juhudi za Serikali katika kufikia jamii na kuleta Maendeleo kwa wananchi kupitia mashirika yenu kwa kufanya kazi bega kwa bega na Serikali kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii.”- Mkurugenzi Mji Mafinga.
Kikao cha Robo ya kwanza kwa Asasi zisizo za Kiserikali(NACONGO) ngazi ya Wilaya kimefanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji Mafinga.
Akizungumza Ndugu Fidelis Filipatali Mwenyekiti wa Baraza la Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NACONGO) amesema Mkutano huu wa Robo ni muhimu kwa Taasisi kwakuwa kupitia kikao hiki kazi zinazofanywa na Taasisi hizo zitajulikana na changamoto yoyote itatatuliwa kwa ushirikiano wao na Serikali.
Kikao hicho kimehudhuriwa pia na wataalamu kutoka Idara ya Maendeleo ya Jamii na Taasisi mbalimbali kutoka katika Wilaya ya mufindi.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.