Baraza la Waheshimiwa Madiwani likiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Mheshimiwa Regnant Kivinge, Watumishi wa Halmashauri wakiongozwa na Mkurugenzi wa Mji Bi, Fidelica Myovella @fidelicagabrielmyovella wanawatakia Heri wanafunzi wa Kidato cha sita wanaotarajia Kuanza Mtihani Taifa wa kumaliza kidato cha Sita tarehe 6/5/2024 Mpaka tarehe 24/5/2024.
Akizungumza Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Mji Mafinga Mwalimu Stephen Shemdoe amesema katika Halmashauri ya Mji Mafinga jumla ya Watahiniwa 427 wanatarajiwa kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita ambapo wavulana ni 249 na Wasichana ni 178 .
Mwalimu Shemdoe amesema Watahiniwa hao 427 wanatoka katika Shule za Serikali 2 na Shule Binafsi 6. Amesema katika Halmashauri ya Mji Mafinga vipo vituo 8 vya kufanyia Mtihani huo wa Taifa.
Nae Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi, Fidelica Myovella anawakumbusha wazazi na walezi wa Watahiniwa hao kuhakikisha wanawasaidia ili waweze kufanya mitihani yao na kumaliza salama tarehe 24/5/2024 bila vikwazo vyovyote.
Imeandaliwa na Sima Bingileki
Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano Serikalin
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.