“Sisi watumishi wa Afya tumebeba dhamana ya Afya za wananchi wa Mafinga,
Tuzuie mapema milipuko ya magonjwa na kukinga kuliko kutibu ni gharamq”
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Mji Mafinga Bi Fidelica Myovella alipokuwa akizungumza na Wahudumu wa Usafi wa Halmashauri ya Mji Mafinga lengo likiwa ni kupokea Changamoto zao kuzitatua kwa lengo la kuboresha Haki zao na kuboresha mazingira ya Usafi katika Halmashauri ya Mji Mafinga.
Amesema Mji umekuwa ukipongezwa katika Sekta Mbalimbali ikiwemo Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo, Elimu, Afya na Usafi wa Mazingira hivyo lazima tujue nani anasababisha tupigiwe makofi na nani anafanya tusipigiwe makogi kwemye Usafo wa Mazingira.
“ Nimepokeq Changamoto zenu zote na ninaahidi kuzifanyia kazi ntawaita tena na mtaona mabadiliko kuanzia sasa mimi na Timu ya Menejimenti yanayotakiwa kufanyiwa kazi haraka tunafanya na yanayohitaji maamuzi ya Waheshimiwa Madiwani basi tutayaeasilisha ili watolee majibu.”
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Mheshimiwa Regnant Kivinge amesema kuweka mikakati kama hii kunasaidia kuendelea kuweka mji safi na kupunguza magonjwa yanayoweza kusababishwa na uchafu ambapo lengo ni kuzuia milipuko ya magojwa , hivyo amesisitiza kushirikiana zaidi kwenye kazi na kuendelea kuwa wazalendo.
Kikao hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri kimehudhuriwa na Wahudumu wa Usafi, Watendaji wa Kata, Watendaji wa Mitaa, Wenyeviti wa Mitaa, Madereva wa magari ya Taka na baadhi ya wakuu wa Idara
Na Sima Mark Bingileki
Afisa Habari Mkuu-Mafinga TC
wafanyakazi wa kada ya usafi na mazingira wakimsikiliza Mkurugenzi Bi Fedelica Myovella.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.