Kauli hiyo imetolewa na Afisa Mwandikishaji Jimbo la Mafinga Mjini Ndugu Charles Mwaitege akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi Fidelica Myovella walipokuwa wakitembelea na kukagua zoezi la uandikishaji katika vituo vya Uandikishaji Wapiga Kura katika Kata 9 za Halmashauri ya Mji Mafinga.
Vituo vilivyokaguliwa na kutembelewa ni Ofisi ya Mtaa wa Igawa, Lutalawe,Chogo na Malingumu.
Afisa Mwandikishaji Jimbo la Mafinga Mjini Ndugu Charles Mwaitege amesema vituo vinafunguliwa kuanzia saa 2 kamili Asubuhi na kufungwa saa 12 kamili jioni .
Aidha amewawataka wananchi wote wanaotakiwa kuandikishwa na kuboresha taarifa zao watumie siku hizi vizuri ili kuweza kujiandikisha kupata kadi ya Mpiga Kura zoezi linalosimamiwa na Tume huru ya Uchaguzi
Sima Bingileki
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mafinga TC
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi Fedelica Myovella akikagua vituo mbalimbalui na kuangalia zoezi la uwandikishaji na uboreshaji wa taarifa kwenye daftari la kudumu la mpiga kura jimbo la Mafinga Mjini.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.