Leo tarehe 6 Januari 2025 Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Dkt. Linda Salekwa akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Mufindi ameitisha kikao kilichowahusisha Wakurugenzi, Wenyeviti wa Halmashauri pamoja na Wajumbe wa Timu ya Menejimenti lengo likiwa ni Kujadili na kujua Mipango na Mikakati ya Ukusanyaji wa Mapato kwa Nusu ya pili ya Mwaka wa fedha 2024/2025) na kubuni vyanzo vipya vya mapato kwa mwaka ujao wa fedha 2025/2026
“Tunatamani kujua kila Halmashauri imejipangaje katika Kubaini vyanzo vipya vya Mapato, hali ya ukusanyaji wa mapato na mikakati kwa bajeti ijayo ya mapato, tuhakikishe tunaupanga Mji, kutafuta wawekezaji kwenye maeneo ya michezo na kuja na mkakati wa shopping mall ili makampuni na taasisi wawekeze hapo katika kukuza uchumi wa Halmashauri zetu na kuongeza Mapato”
Akizungumza Katibu Tawala wa Wilaya ya Mufingi ndugu Reuben Chongolo Amesema kuwa kikao kitaleta Tija kwa Halmashauri na Wilaya kwani kitafungua njia kwa mawazo ya kubuni vyanzo vipya vya mapato kuongeza mikakati ya kuongeza mapato.
Kikao hicho cha kujadili kuongeza mapato kwa Halmashauri kimehudhuriwa na Wakurugenzi wa Halmashauri akiwepo Bi. Fidelica Myovella, Kamati ya Ulinzi na Usalama na Wajumbe wa Timu ya Menejimenti wa Halmashauri zote mbili za Wilaya ya Mufindi
Imeandaliwa na
Sima Mark Bingileki
Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini- Mafinga TC
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na usalama wa Wilaya ya Mufindi na wajumbe wa Halmashauri ya Mji Mafinga wakifatilia kikao cha Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Dkt Linda Selekwa juu ya ukasanyaji wa mapato.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.