Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Dkt. Linda Salekwa amewataka wanawake kujitathmini hususan katika malezi ya watoto. Amesema wazazi wengi hawazungumzi na watoto kiasi kwamba watoto wanakosa kupata mafunzo kutoka kwa wazazi na hata wakifanyiwa vitendo vya ukatili wanashindwa kuwaambia wazazi kwa kuwa wazazi wengi hawana muda wa kuzungumza na watoto wao.
“ wakina mama tujitathmini, jukumu la kulea watoto ni letu, tusiwaachie kina baba, mama tenga muda wa kumjua mwanao ukiona mabadiliko yoyote ujue, tuwe marafiki wa watoto wetu, ili waweze kutuambia wakifanyiwa ukatili” tutenge muda wa kuzungumza nao”
Aidha amemshukuru Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kutambua nafasi ya mwanamke hivyo kuwaomba wanawake wasimuangushe mheshimiwa Rais kwani tayari kawathamini wanawake basi na wanawake waonyeshe thamani yao kwa kuheshimiwa na Rais
Sherehe za maadhimisho ya siku ya wanawake wilaya ya Mufindi imefanyika kata ya Ikongosi na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali na wananchi kutoka Halmashauri ya Mji Mafinga na Halmashauri ya Mufindi.
Burudani mbalimbali zilikuwepo, mashirika yasiyo ya Kiserikali na wajasiliamali mbalimbali waliokuwa wakionyesha bidhaa ziluzopitiwa na kukaguliwa na Mheshimiwa Mgeni Rasmi.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI- MAFINGA TC
Sima Bingikeki
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini- Mafinga Tc
Halima Dendego
Angela Kairuki
Ofisi ya Rais - Tamisemi
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.