Maafisa Bajeti wa Divisheni na Vitengo, Maafisa TEHAMA na Manunuzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga wameanza mafunzo ya siku 5 kuhusiana na matumizi ya Mfumo wa Manunuzi wa Kielekroniki Serikalini( NeST)Mjini Mafinga.
Akizungumza Mkuu wa Kitengo chaUsimamizi wa Ununuzi Halmashauri ya Mji Mafinga Ndg. Honest Mlambo amesema Mafunzo haya ya siku 5 mfululizo kwa Maafisa Bajeti wa Divisheni na Vitengo yatasaidia kupunguza hoja za Ukaguzi na yataboresha Manunuzi ya Umma na baada ya Mafunzo Halmashauri itaanza kutumia mfumo huu wa NeST ulioboreshwa kuanzia tarehe 1/10/2023
Aidha amesema kuwa Mafunzo haya pia yatatolewa kwa Wakuu wa Divisheni na Vitengo kuanzia tarehe 13/9 mpaka tarehe 19/9.
Mfumo huu mpya wa Manunuzi wa Kielektroniki Serikalini(NeST) utaanza kutumika rasmi kuanzia tarehe 1/10/2023 ikiwa ni mbadala wa Mfumo wa awali uliokuwa unajulikana kwa jina la TaNePS.
Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Ununuzi wa Umma( PPRA) ndio msimamizi wa Mfumo huu mpya wa Kielektroniki Serikalini( NeST)
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini- Mafinga TC
Sima Bingikeki
Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini-Mafinga TC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.