Halmashauri ya Mji Mafinga ni moja kati ya Halmashauri zinazoongoza kwa ufaulishaji mkubwa wa Elimu ya awali,msingi na sekondari katika mkoa wa Iringa kwa miaka kwa miaka mitatu mfululizo ukilinganisha na Halmashauri nyingine ndani ya Mkoa.
Akitoa taarifa Afisa Elimu Taaluma Mji Mafinga Ndugu, Kasmiri Sambala kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga.
Amesema mambo yanayochangia kuongezeka hali ya ufaulishaji Mji Mafinga ni pamoja na hali nzuri ya miundo mbinu katika shule ,idadi ya walimu na upatikanaji wa chakula mashuleni kwa upande wa divisheni ya elimu ya awali na msingi.
Aidha ameongeza kuwa fursa zinazochangia ufaulishaji ni pamoja na utekelezaji wa mtaala na uboreshaji wa taaluma katika Halmashauri ya Mji Mafinga ni kuwatumia Wadau mbalimbali wa Elimu waliopo katika Halmashauri yetu ambao wanasaidia kuwajengea uwezo walimu kwenye ufundishaji na ujifunzaji kufanya hivyo ubora wa taaluma umekuwa ukiongezeka.
Nae Afisa Elimu Mkoa wa Tabora ,Ndugu Juma Japhet Kaponda ameipongeza Halmashauri ya Mji Mafinga katika suala zima la ufaulishaji kuna kitu cha kujifunza.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Mkurugenzi wa Mji Mafinga Bi Happiness laizer, Wakuu wa divisheni mbalimbali Mji Mafinga na Maafisa Elimu kutoka Mkoa wa Tabora.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
Christopher Mhina
Mwandishi wa Habari Mafinga TC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.