Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Ndugu, Peter Ngusa amekabizi Vishikwambi 13 kutoka Wizara ya Mifugo na Uvivu kwa ajili ya Maafisa Mifugo 13 wa Halmashauri ya Mji Mafinga kwa ajili ya zoezi la kuchanja na kutambua ngo’mbe ambapo kwa Halmashauri ya Mji Mafinga inatarajia kuhudumia Ng’ombe elfu 10,000.
Akizungumza na Maafisa Mifugo wa Halmashauri ya Mji Mafinga kwanza ameishukuru Wizara ya Mifugo na Uvivu kwa kuwapatia vifaa hivyo na pia amewasisitiza utunzwaji mzuri wa Vishikwambi kwani ata baada ya zoezi vitabakia kwa ajili ya matumizi mengine ya ofisi hivyo vinapaswa kutunzwa vizuri.
Na,
Anna Mdehwa,
Afisa Habari.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.