Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kaona haitoshi kujenga Miundombinu ya Hospitali pekee sasa katuletea Madaktari bingwa 7 ambao kuwepo kwao kutapunguza gharama za wananchi kufuata huduma za kibingwa mbali na kuimarisha Afya za wananchi kwa matibabu ya kibingwa yatakayotolewa katika Hospitali ya Mji Mafinga kuanzia tarehe 2-6/6/2025”
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu Wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Dkt. Linda Salekwa alipokuwa anawapokea Madaktari bingwa 7 katika Hospitali ya Mji Maginga.
Amewataka wananchi wa Wilaya ya Mufindi na Halmashauri ya Mji Mafinga kuhakikisha wanazitumia siku hizi muhimu ili waweze kupata huduma za madaktari bingwa ambao wamekuja kwa Mpango Maalumu wa Rais ya kuhakikisha wananchi wote mpaka pembezoni wanapata huduma za kibingwa kwa gharama nafuu na kuimarisha Afya za watanzania bila kuwafuata mabingwa mbali.
Akiwatambulisha Madaktari hao bingwa maarufu kama Madaktari wa Mama Samia Daktari wa Mji Mafinga Bonaventulla Chitopela amesema Timu ina jumla ya madaktari 7 akiwemo Bingwa wa magonjwa ya Wanawake na Ukunga, Meno, Mfumo wa Mkojo, magonjwa ya ndani, bingwa wa magonjwa ya watoto na bingwa wa magonjwa ya dharula ambapo watatoa huduma za kibingwa kuanzia saa 2.00 Asubuhi mpaka saa 10.30 jioni katika Hospitali ya Mji Mafinga.
Naye Kiongozi wa Timu hiyo ya Madaktari Bingwa Dkt Huruma Mwasipu ambaye ni
Daktari bingwa wa magonjwa ya dharula amesema wapo tayari kutoa huduma kama ambavyo imekusudiwa hivyo wananchi wenye kuhitaji huduma hiyo wafike kwa wingi katika Hospitali ya Mji Mafinga.
Nao wananchi Irene Kadinde wa Mji mwema Mafinga na Tausi Mbalamwezi wamesema hakika mama Samia anajali wananchi wake, huduma hizi eangezipata kwa kuzifuata mbali ila mabingwa wapo mafinga hakika mama kweli ni msikivu na anajali Afya za wananchi wake”
Mapokezi ya madaktari bingwa maarufu kama Madaktari wa Mama Samia Suhulu Hassan yamehudhuriwa pia na Mkurugenzi Mji Mafinga Bi, Fidelica Myovella, Madaktari wa Mji Mafinga pamoja na wananchi waliofika kupata huduma za madaktari bingwa.
Sima Bingileki
Afisa Habari Mkuu- Halmashauri ya Mji Mafinga
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.