Kila kada ni muhimu kwa Ustawi wa Halmashauri na Utekelezaji wa Majukumu ya Serikali, hivyo hakikisheni kwenye utekelezaji wa majukumu yenu ya Udereva mnatimiza wajibu wenu kwani magari yenu ndio ofisi zenu, fanyeni kazi kwa kufuata maadili ya kazi zenu”
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mji Mafinga Bi Fidelica Myovella alipokuwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Mji mafinga kada ya Madereva lengo likiwa ni kusikiliza changamoto zao na kuzitatua sambamba na kuwakumbusha kuhusu utendaji wa kazi zao kwa kufuata sheria na kanuni za Utumishi wa Umma.
Amesema watumishi hao wa kada ya udereva wamekumbushwa kuhusu ujazaji wa logbook, matumizi sahihi ya mafuta, utunzaji wa magari, uadilifu na lugha sahihi za mawasiliano.
Aidha Mkurugenzi Bi. Fidelica Myovella ameahidi kutatua changamoto zilizowasilishwa na watumishi hao wa Kada ya Udereva.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu Ndugu Charles Mwaitege, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi Bi Tunu Bushiri, Afisa Usafirishaji Mji Mafinga na Wakuu wa Idara na Vitengo.
Sima Bingileki
Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini Mafinga TC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.