Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Mhe, Regnant Kivinge amewapongeza wataalamu wa Mji Mafinga kwa kuaandaa bajeti ambayo inaenda kutatua kero kwa Wananchi na amewaasa kutekeleza bajeti kama ambavyo imepangwa.
Kwa pamoja Madiwani wamepitisha Rasimu ya Mpango wa bajeti 2025/2026 ambapo wamepongeza ongezeko la bilioni moja kwenye makusanyo ya mapato ya ndani ambapo imefikia bilioni 7.6.
Aidha Mhe, Makoga Diwani wa kata ya Isalavano akizungumza kwa niaba ya Madiwani amepongeza kutengwa shillingi milioni hamsini kwa ajili ya kusimamia miradi ya maendeleo na pia mafunzo kwa Watumishi kwani itasaidia kuongeza ufanisi katika kazi.
Pia Eng. Richard Sanga Meneja Wilaya ya Mufindi TARURA amewasilisha Rasimu ya Mpango wa Bajeti ambayo inazaidi ya Bilioni kumi na moja yenye lengo la kuboresha na kujenga barabara katika Mji wa Mafinga ambapo kwa pamoja Madiwani waliipitisha.
Aidha MAUWASA wameeleza miradi mbalimbali ya maji inayoenda kutekelezwa katika Halmashauri ya Mji Mafinga kwa Mwaka wa fedha 2025/2026 ambapo Madiwani wamepitisha Rasimu ya Mpango wa Bajeti iyo inayoenda kutatua kero ya maji kwa Wananchi.
Madiwani wakisikiliza uwasilishaji wa bajeti ya Halmashauri ya Mafinga Mji.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.