Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Reginant Kivinge kwa niaba ya Madiwani wote baada ya kuadhimia kwa pamoja kumuunga mkono kwa kazi nzuri ambayo ameifanya si katika Halmashauri ya Mji Mafinga peke yake bali Tanzania kwa ujumla.
“Sisi tunaunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais tunatambua kazi kubwa anayofanya kwa mfano Halmashauri ya Mji Mafinga zimeletwa fedha za Miradi ya Maendeleo na Shule mpya 8 zimejengwa kama shule ya Amali imegharimu zaidi ya Bilioni 1.6 na mengine mengi” Amesema Reginant Kivinge.
Pia amewaomba watu washiriki uchaguzi na kuwaomba Wananchi wampigie kura Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na kuendelea kumuunga mkono.
Mkutano huo wa Baraza la Waheshimiwa Madiwani( Robo ya tatu) Januari - Machi. Pia walijadili na kupitisha taarifa za Kamati mbalimbali.
Na
Anna Mdehwa
Afisa Habari
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.