MAFINGA MJI MABINGWA WA VOLLEYBALL(wanaume) NA MABINGWA WA KURUSHA TUFE( Wanawake) SHIMISEMITA 2003.
Halmashauri ya Mji Mafinga imeibuka BINGWA wa Mchezo wa Volleyball wanaume na Kurusha Tufe kwa wanawake katika Michezo ya SHIMISEMITA Taifa 2023 iliyofungwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu Dkt.Charles Msonde katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Katika Michezo Hiyo iliyoanza tarehe 18-31/2023 jumla ya Halmashauri 70 kati ya Halmashauri 184 zimeshiriki Michezo hiyo Iliyoandaliwa na Shirikisho la Michezo Serikalini za Mitaa(SHIMISEMITA).
Dkt Msonde amesema wakurugenzi wote wa Halmashauri wahakikishe wanatenga Bajeti ya kutosha ili mwakani 2024 Halmashauri zote zipeleke Timu kwenye Michezo hiyo kwani inarudisha hari ya utendaji kazi, kuimarisha Afya kujenga mahusiano na zaidi kuzitangaza Halmashauri .
Naye Mwenyekiti wa SHIMISEMITA TAIFA Ndugu Jeshi Lupembe ameshukuru ushirikiano mkubwa uliotolewa na Ofisi ya Rais TAMISEMI, Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Kamati Tendaji ya Shirikisho, Halmashauri zilizoshiriki na Wadau wa michezo kwa kufanikisha Michezo hii na kutangaza Mkoa wa Mwanza kuwa wenyeji wa Michezo SHIMISEMITA 2024.
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Mafinga TC
Sima Bingileki
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano-MafingaTC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.