Halmashauri ya Mji Mafinga inayoongozwa na Bi. Fidelica Myovella kwa mchezo wa Mikakati na Maarifa Makubwa imeweza kuishusha milima Timu ya wanaume ya Hanang kwa seti 2-0 Mchezo uliokuwa wa vuta nikuvute katika viwanja vya Tanga Tech
Mchezo huo uliochezwa saa kumi jioni umevuta hisia za watu wengi kulingana na umahiri wa Timu zote mbili ambazo hazikuwa radhi kupoteza mchezo huo.
Akizungumza kocha wa Timu ya wanaume kwa mpira wa wavu, ‘Rapha’ amesema mchezo ulikuwa ni mgumu kwani timu zote zilipanga kuchukua ushindi japo Timu yw Mafinga ilikuwa na mikakati na kurekebisha pale walipokuwa wanashauriwa kufanya hivyo.
Mpaka sasa Timu ya wanaume kutoka Mafinga imecheza michezo 4 imepoteza mmoja na kushinda michezo mitatu.
Na Sima Bingileki
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.