"Tuendelee kutoa Elimu ili wananchi wajitokeze kwa wingi kujiandikisha katika Orodha ya Wapiga Kura kwaajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa tarehe 27/11/2024 na tuhakikishe katika zoezi la kujiandikisha vituo viwe wazi kuanzia saa 2 Asubuhi na kufungwa saa 12 Jioni , isifike saa mbili asubuhi ndo kituo kianze kufunguliwa hii sio sawa ni kuwanyima haki wananchi na kuvunja kanuni za Uchaguzi.Kituo kinatakiwa ifikapo saa mbili asubuhi kituo kipo wazi na wananchi wanaanza kujiandikisha”
Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 30/9/2024 na Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi. Fidelica Myovella @fidelicagabrielmyovella alipokuwa akifungua mafunzo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 kwa wasimamizi wasaidizi ngazi ya Halmashauri, Kata, Mitaa na Vijiji yaliyofanyika katika ukumbi wa TRC Mafinga.
Naye Mratibu wa Uchaguzi Halmashauri ya Mji Mafinga Ndugu Benedict Kibiki amesema mafunzo haya ni mafunzo ya siku moja kwa wasimamizi 60 yenye lengo la kuwapa mafunzo wasimamizi wa Mitaa, Wasimamizi wa Vijiji na Wasimamizi wasaidizi wa Kata na Wasimamizi wasaidizi ngazi ya Wilaya kufahqmu kanuni katika kusimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uandikishaji wa Orodha ya Wapiga Kura.
Akitoa neno la Shukurani Bi, Imara Mbeha Msimamizi Ngazi ya Mtaa Ivambinungu amesema wapo tayari kuşimamia Uchaguzi na kufuata taratibu, Kanuni na Miongozo yote ya Uchaguzi na Uandikishaji. Tutahamasisha wananchi na kuhakikisha VITUO vinafunguliwa na kufungwa kwa wakati sahihi.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.