Halmashauri ya Mji Mafinga imepokea kiasi cha shilingi 583,180,028.00 kutoka Serikali Kuu kwaajili ya Ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari Katika Kata ya Boma chini ya Mradi wa (SEQUIP)na Fedha kiasi cha shilingi Milioni 100 kwaajili ya Ujenzi wa nyumba za watumishi (2 in 1)katika shule Mpya Kata ya Saohill.
Miradi hii inatekelezwa nchi Mzima ambapo Ofisi ya Rais- TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inaendelea na utekelezaji wa Mradi wa Kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP), Pamoja na shughuli nyingine, mradi unahusika na ujenzi wa shule mpya za Sekondari za Kata.
Akizungumza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Ndugu Ayoub Kambi amesema Shule mpya ya Sekondari itajengwa Kata ya Boma na majengo yatakayo jengwa ni pamoja na :-
-Jengo lenye vyumba vya madarasa 2
-Jengo lenye vyumba vya madarasa 2 na Ofisi 1
-Jengo la Utawala
-Jengo la Maabara ya Kemia na Baiolojia
-Jengo la maabara ya Fizikia
-Maktaba
-Chumba cha TEHAMA
-Jengo la vyoo vya wavulana matunda 4 yakiwa na huduma kwa wenye mahitaji maalum.
-Jengo la vyoo vya wanafunzi wasichana matundu 4 yakiwa na huduma kwa wenye mahitaji maalum na chumba maalum
-Kichomea taka
Na Tanki la maji la ardhini.
Ameongeza kuwa katika fedha zilizopokelewa milioni 100 imeelekezwa kujenga nyumba ya walimu 2 in 1 katika Kata ya Saohill .
Aidha ndugu Kambi amemshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Serikali kwa kuendelea kuleta Fedha katika Halmashauri ya Mji Mafinga katika Sekta Mbalimbali ili kuendelea kuboresha Huduma kwa wananchi .
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI- MAFINGA TC
Sima Bingileki
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini- Mafinga TC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.