Na. Sima Bingileki
Miko ya Mwanza,Mara na Lindi imeng’ara katika mchezo wa riadha wasichana na Wavulana katika mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Tanzania kwa Shule za Msingi inayoendelea Mkoani Iringa.
Mikoa hiyo imeshindana leo juni 13,2025 kwenye viwanja vya Chuo cha ualimu Kleruu, katika hatua za riadha fainali mita 100 Wasichana na wavulana, kupokezana vijiti mita 400 na kurusha mkuki.
Mratibu wa Mchezo wa riadha UMITASHUMTA/UMISSETA 2025 Bi Neema Chongolo, amesema kuwa washiriki wote wana matarajio makubwa ya kushinda, huku akielezea Mara, Mwanza, Lindi na Geita kuwa iliongoza katika michezo ya leo.
“Hakika mikoa yote imejiandaa vizuri kushiriki mchezo huu wa riadha ambao mara zote unakuwa na ushindani mkubwa kutokana na washiriki kujiandaa kushinda, tutarajie ushindani mkubwa kwenye fainali ya mchezo huu” amesema Neema Chongolo
Mashindano ya UMITASHUMTA yalifunguliwa rasmi tarehe 9 Juni 2025 na Wazir Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, na yanaendelea kushika kasi katika viwanja vya Kichangani, Shule ya Sekondari Lugalo,Shule ya Sekondari ya Wasichana Iringa na Chuo cha Kleruu.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.