“Mashindano haya ya UMITASHUMTA na UMISSETA kitaifa katika Mkoa wa Iringa yanafanyika kwa mara ya kwanza Iringa ikiwa ni historia katika Mkoa wa Iringa ambapo itawapa fursa washiriki na wageni kutoka Mikoa yote 26 kutembelea vivutio vya Utalii pamoja, kukuza fursa za kiuchumi kwa wananchi wa Iringa na Mikoa ya Jirani.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Peter Serukamna alipokuwa Akitoa salamu za Mkoq kwenye Ufunguzi wa Mashindano ya UMITASHUMTA na UMISETA Kitaifa Katika Mkoa wa Iringa ambayo yanafunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa.
Amesema Mashindano haya yatafanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Iringa,Shule ya Sekondari ya Lugalo na Viwanja vya Chuo Cha Waalimu Kreluu na kuhudhuriwa na zaidi ya wanafunzi 7,000 kutoka Mikoa 26 Tanzania Bara.
Aidha ameitaja michezo itakayo shindaniwa kuwa ni Soka mpira wa kikapu, mpira wa kengele, wavu, pete naMichezo ya fani za ndani ikiwamo ngoma kwaya.
Ufunguzi wa Mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA Kitaifa katika Mkoa wa Iringa yamehudhuriwa na Waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Palamagamba Kabudi, Ndugu Salim Abri Mjumbe wa Kamati Kuu Wabunge, Wakurugenzi wa Wizara, Maafisa wa Wizara, Wanamichezo , Makatibu Tawala na Wakuu wa Wilaya na Mkuu wa Wilaya yq Mufindi Mheshimiwa Dkt. Linda Salekwa.
Michezo ya UMITASHUMTA NA UMISSETA 2025 inaongozwa na Kauli mbiu “ Viongozi bora ni Msingi wa Maendeleo ya Taaluma, Sanaa na Michezo, Shiriki Uchaguzi Mkuu 2025 kwa Amani na Utulivu”
Na Sima Bingileki
Afisa Habari Mkuu- Mafinga
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.