Leo tarehe 25/4/2025 wameapishwa Mawakala wa Vyama Vya Siasa kwaajili ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya Pili unaotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 1/5/2025 mpaka tarehe 7/5/2025 katika Halmashauri ya Mji Mafinga Jimbo la Mafinga Mjini.
Akizungumza Afisa Mwandikishaji JImbo la Mafinga Mjini Ndugu Charles Mwaitege kabla ya kuapisha Mawakala wa Vyama vya Siasa amesema zoezi litakuwa la siku 7 linalosimamiwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na vituo vitakuwa katika Kata zote 9 za Halmashauri ya Mji ambapo kutakuwa na vituo 30 na vitafunguliwa kuanzia saa 2 kamili asubuhi na Kufungwa saa 12 Jioni.
“ Niwaombe sana wale ambao walishindwa kuboresha taarifa zao au walishindwa kujiandikisha kipindi cha nyuma watumie fursa hii ili waweze kujiandikisha na wawahi kwenye vituo wasisubiri siku ya mwisho ndo wajitokeze kwa wingi. Charles Mwaitege Afisa Mwandikishaji Jimbo la Mafinga Mjini
Akizungumza Mratibu wa Uchaguzi Halmashauri ya Mji Mafinga Ndugu Benedict Kibiki amesema vituo vitafunguliwa saa 2 kamili Asubuhi na kutakuwa na vituo 30 . Hivyo amewaomba wananchi ambao hawajaboresha taarifa zao kujitokeza kuanzia siku ya kwanza wasisubiri siku ya mwisho.
Mawakala wa vyama walioshiriki kula kiapo ni Chama Cha Mapinduzi ( CCM) na Chama Cha ACT
Imeandaliwa na
Sima Bingileki
Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano Mafinga TC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.