Maafisa Habari ni Nguzo ya Maamuzi ya Kuwalisha taarifa Sahihi kwa wananchi na kuamua nini kinaenda kwenye jamii kwa kuhakikisha hakuna taarifa za upotoshaji kuhusu kazi zilizofanywa na Serikali ambazo hazitolewi ufafanuzi”
Kauli ya Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI alipokuwa Akizungumza na Maafisa Habari wa Halmashauri na Mikoa kwenye Kikao Kazi cha siku 2 cha Maafisa Habari Jijini Dodoma
Amesema kila Afisa Habari akisimama kwenye nafasi yake Kazi zote nzuri zinazofanywa na Serikali hasa Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo zitatangazwa na wananchi mpaka ngazi ya Mtaa watafahamu nini Serikali imefanya kwenye maeneo Yao.
“ Maafisa Habari, tusikae kimya tutangaze kazi za Serikali na tuisemee Serikali popote inaposemwa tofauti kwenye maeneo yetu, kwa kufanya hivi tuta kuwa tunatangaza kazi za Serikali za Utekelezaji wa Miradi”
Mhe Mchengerwa amesema kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 Ofisi ya Rais TAMISEMI imepitishiwa bajeti ya Shilingi 11,782,984,202,000.00 ambazo zinakwenda kutekeleza Miradi kwenye Halmashauri, MIKOA na Taasisi hivyo kuwataka Maafisa Habari kuwa wazalendo katika kutangaza utekelezaji wa miradi kwenye maeneo Yao pindi inapoanza utekelezaji.
Mada mbalimbali zimewasilishwa katika kikao hicho ikiwamo mada kutoka Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mawasiliano ya Kimkakati, umuhimu wa kufahamu Mlaji wa habari anataka nini, Afya na Elimu.
Maafisa Habari kutoka Halmashauri ya MJI Mafinga wamehudhuria kikao hicho.
Na Sima Bingileki
Afisa Habari Mkuu- Mji Mafinga
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.