Naibu waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe(Mb) ameelekeza Mikoa yote kuainisha maeneo ya uwekezaji na kuyatangaza ili wawekezaji wakifika nchini wakute mazingira wezeshi kuwekeza ,kukuza utalii na uchumi wa nchi bila urasimu kwani maeneo tayari yanakuwa yapo yamepimwa miundombinu yote ipo na yanafahamika.
Amesema kila Mkoa na wilaya uandae mikakati ifuatayo ili kuweza kukuza uchumi, kuendeleza utalii na kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji.
-Mikoa na Halmashauri zake ziendelee kutangaza fursa za Utalii katika Mikoa yake.
-Kuibua mazao ya Utalii na Kuendeleza kutangaza vivutio vya utalii kusini.
-Timu za Uratibu ufanyike kwa pamoja ili kuweza kuandaa kwa ufanisi Maonesho ya Karibu Kusini.
Aidha Naibu Waziri Kigae amewataka watanzania kuwekeza katika hotel za nyota 5 ili kuweka mazingira mazuri ya wageni na wawekezaji na kukuza uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Akizungumza wakati wa kumkaribisha Mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Halima Dendego amesema Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amekuwa kinara na Balozi namba moja katika kutangaza na kukuza Utalii hivyo, Maonesho haya ya Utalii Karibu Kusini ni jitihada za kuunga mkono juhudi za mhshimiwa Rais katika kutangaza vivutio vya Utalii Karibu Kusini.
“ Maonesho haya yamekuwa na mafanikio makubwa sana kwa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kwani sasa mikoa hii 10 ambayo inaratibu Maonesho haya vivutio vyake vinatangazwa na watalii wanakuja kwa wingi kutembelea vivutio hivi. Mpakq leo tunapoenda kufunga maonesho haya tumepata waoneshaji 135 kutoka sehemu mbalimbali nchini hata nje ya Mipaka ya Tanzania. hakika tunajivunia”
Katika Maonesho haya ya Karibu kusini Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii limeibuka banda bora la Jumla, Mkoa ulioibuka kidedea katika sekta ya Mikoa ni mkoa wa Njombe na Wizara iliyoibuka mshindi upande wa wizara ni wizara ya Maliasili na Utali.
Maonesho haya yamepambwa na burudani mbalimbali ikiwamo mashindano ya magari , pikipiki na ngoma za utamaduni kutoka nyanda za juu kusini.
Maonesho haya ya Utalii Karibu Kusini yalizinduliwa tareheb23/9/2023 na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Angellah Kairuki(Mb) katika Viwanja vya kihesa Kilolo Iringa.
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini- Mafinga TC
Sima Bingileki
Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano- Mafinga TC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.