Miradi hii ipo katika hatua ya ukamilishaji na tunahakikisha mafundi hawapati Changamoto ya Vifaa katika Utekelezaji wa Miradi”
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mji Mafinga Bi. Fidelica Myovella alipokuwa akifanya Ufuatiliaji wa Miradi ya Maendeleo ya ujenzi wa Shule ya Sekondari katika Kata ya Upendo na Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Amali( Ufundi)Changarawe
Amesema kuna baadhi ya Majengo ambayo tayari yamekamilika katika Miradi hii na kuna baadhi ya majengo yanaendelea kukamilishwa, kwa hatua tuliyofikia yatakamilika kwa wakati.
“ Ndoto za Rais Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan ni kuona wanafunzi wanapata mazingira mazuri ya Elimu nchini Tanzania, hivyo kuamua kuleta fedha nyingi katika Sekta hii, lazima tusimamie Miradi hii na kuhakikisha inakamilika kwa wakati “
Serikali imeleta fedha kiasi cha Shilingi Bilioni 1.6 kwaajili ya Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Amali katika Kata ya Changarawe yenye majengo 19, Shule hii itasaidia wanafunzi wa Mafinga na Tanzania kwa ujumla kupata Elimu ya Sekondari na Ufundi mafinga.
Imeandaliwa na Sima Bingileki
Afisa Habari Mkuu Halmashauri ya Mji Mafinga.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.